Wananchi wakishuhudia baadhi ya nyumba zilizofunikwa na maporomoko hayo.
WATU 10
wamepoteza maisha huku zaidi ya 300 wakiwa hawajulikani walipo baada ya
kutokea maporomoko ya udongo katikati mwa nchi ya Sri Lanka leo.
Maporomoko
hayo yametokea kufuatia kunyesha kwa mvua kubwa ambapo takribani nyumba
140 zimefunikwa na udongo katika Wilaya ya Badulla.
Msemaji wa Kitengo cha Kukabiliana na Maafa nchini humo, Sarath Kumara amethibitisha taarifa hizo.
Msemaji wa Kitengo cha Kukabiliana na Maafa nchini humo, Sarath Kumara amethibitisha taarifa hizo.
Vyombo mbalimbali vya uokoaji vipo eneo la tukio kujaribu kuokoa majeruhi wa tukio hilo.
Maporomoko
hayo pia yamelikumba shamba kubwa la chai la Meeriyabedda lililopo
karibu na mji wa Haldummulla, uliopo kilomita 200 (maili 120) mashariki
mwa mji mkuu Colombo.(P.T)
No comments:
Post a Comment