Na Mwandishi wetu_MAELEZO-Dar es salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa
kituo cha michezo katika eneo la Kidongo Chekundi jijini Dar es salaam.
Kituo cha michezo kinajengwa kwa ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion Power na Serikali ya Tanzania.
Shehere hizo zinatarajiwa kesho asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.
Kwa mijbu
wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa
Symbion nchini Julie Foster , sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Waziri
wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi.
Margaret Byrne na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa ujenzi huo Rais Kikwete
atapanda mti kwenye eneo hilo, akisaidiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Sunderland AFC Bi. Byrne, Mkurugenzi wa Biasharawa klabu hiyo Gary
Hutchinson, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Hinks.(P.T)
Klabu ya
Ligi Kuu ya Uingereza ya Barclays, Sunderland AFC inatoa usaidizi wa
kiufundi na utendaji katika uendelezaji wa mradi wa mpira wa miguu,
ambao ni wa kwanza na wa aina yake nchini humu, utakaohakikisha maelfu
ya vijana wananufaika kutokana na mtazamo wa pamoja wa kuchanganya mpira
wa miguu, elimu na ushiriki wa jamii, ili kupata ujuzi na utaalam wa
Sunderland AFC.
MWISHO
Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na
Julie Foster
0787365495
No comments:
Post a Comment