Rais wa
timu ya Lipuli Jesca Msavatavangu (mwenye kapelo) akisalimia na kikosi
cha Lipuli kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Simba SC ya
Dar es Salaam jana katika uwanja wa samora mjini Iringa, ambapo Simba
ilishinda goli 1 kwa nunge. (Picha na Friday Simbaya)(MM)
Na Friday Simbaya, Iringa
Timu ya
Simba ambayo inajiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya
Mtibwa Suger ya Mkoani Morogoro, siku ya Jumamosi imeonja ladha ya
ushindi baada ya kuifunga timu ya Lipuli (Wanapaluhenge) ya mkoani
Iringa ambayo ipo kwenye maandalizi ya mechi ya ligi daraja la kwanza
dhidi ya Kimondo Fc ya Mkoani Mbeya.
Mchezo
huo ulimalizika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi mwembamba wa goli
moja kwa nunge, mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu
Samora mjini Iringa.
Timu ya
Simba ambayo imeshuka dimbani mara tano kwenye ligi kuu Tanzania Bara
msimu huu na kutoka sare michezo yote huku ikiwa imefunga goli tano na
kufungwa idadi hiyo, inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi
hiyo.
Kocha wa
timu ya SIMBA Mzambia Patrick Phiri, aliutumia mchezo wa jana kama
maandalizi,huku akiwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha vijana cha
timu hiyo.
Timu ya
SIMBA ilianza mchezo taratibu na kuifanya timu ya Lipuli kutawala
kipindi cha kwanza ambapo hadi mapumziko timu hizo
zilikuwa hazijafungana.
Kipindi
cha pili Simba walionekana kubadilila na kuanza kulishambulia kwa kasi
lango la lipuli hatimaye ilifanikiwa kupata goli ambalo lilifungwa na
mshambuliaji hatari Elias Maguli ambae alitumia makosa ya mabeki wa
Lipuli waliochelea kuondoa mpira kwenye eneo lao la hatari.
Kuingia
kwa bao hilo kuliufanya mchezo kuchangamka huku timu
zote zikishambuliana kwa zamu lakini mpaka mwisho wa mchezo Simba
waliibuka kifua mbele.
Baada ya
kumalizika kwa mechi hiyo kocha mkuu wa Wekundu wa msimbazi akiongea na
Waandishi wa habari alitamba kuibuka na ushindi kwenye mechi dhidi ya
Mtibwa akisema vijana wake wameahidi kushinda mchezo huo.
Kuhusu
kupewa mechi mbili na uongozi wa timu hiyo kocha uyo alisema yeye kwa
sasa anaangalia namna ya kushinda michezo yote iliyobaki.
Pia kocha huyo aliimwagia sifa timu ya Lipuli na kusema ni timu nzuri na wametoa upinzani mkali kwa vijana wake.
Kwa
upande wake Rais wa timu ya Lipuli Jesca Msavatavangu alisema vijana
wake walicheza vizuri huku wakionekana kucheza kwa hali na mali, hivyo
kutoa burudani kwa wakazi wa Mjini Iringa na viunga vyake.
Msavatavangu
alisema hiyo ilikuwa ni nafasi kwa vijana wake kuonekana kwa wakazi wa
Iringa ikiwa ni pamoja na kuonyesha kiwango cha soka, kwa kucheza na
timu kubwa zinazoshiriki ligi kuu.
No comments:
Post a Comment