Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari yaKambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar esSalaam,wakioneshwa na Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi yawanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es
Salaam Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi na Mawasiliano wa
Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza (kushoto ) pamoja na Meneja
uhusiano wa umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)
wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya
sekondari ya Kambangwa, Matha Galusaki akielezea jinsi anavyoweza kupata
taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati
walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua maendeleo ya
mradiwa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na
Samsung. Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini
wanaendelea kunufaika na mradi huo.(P.T)
Baadhi ya
Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa
iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo
Theresia Ng’wigulu watatu toka kulia pamoja na maofisa wa Vodacom
Tanzania, Matina Nkurlu wa kwanza kushoto na Renatus Rwehikiza (kulia)
wakimsikiliza Mwalimu wa somo la kompyuta wa kidato cha pili Nicolas
Wilson wa shule hiyo akiwafafanulia jambo kuhusiana na elimu ya mafunzo
ya kompyuta wakati walipotembelewa na maofisa hao kujua maendeleo ya
mradi wa TEHAMA uliofadhiliwana Vodacom Foundation kwa kushirikiana na
Kampuni ya Samsung. Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za
sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
No comments:
Post a Comment