*AANZA ASUBUHI KWA KAZI KIBAO
*MAELFU WAFURIKA KATIKA MKUTANO WAKE IRINGA MJINI
*MAKATIBU WATATU CHADEMA WAHAMIA CCM
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi kwenye
Uwanja wa Mwembetogwa, leo Oktoba 11, 2014, mwishoni mwa ziara yake ya
kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Iringa
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Katibu wa Chadema jimbo la
Mufindi Kusini, Emmanuel Ngaladi baada ya kupokea kadi yake ya Chadema,
hatua iliyofuatiwa na kutangaza kwake kuhamia CCM katika mkutano huo
uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo
Katibu
wa Chadema, jimbo la Mufindi Kusini akitangaza kukihama Chadema na
kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika leo,
Mwembetogwa, Iringa mjini. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye aliyempandisha jukwaani kutangaza uamuzi huo
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi kutoka kwa Katibu Mwenezi
wa Chadema katika Chuo Kikuu cha Sebastiab Koloa, Tanga, Mdillah
Osward ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano huo
uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo
Katibu
Mwenezi wa Chadema katika Chuo Kikuu cha Sebastiab Koloa, Tanga,
Mdillah Osward, akitangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM katika
mkutano huo wa
hadhara uliofanyika leo, Mwembetogwa, Iringa mjini. Kulia ni Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyempandisha jukwaani kutangaza
uamuzi huo
Kada machachari na msomi wa Chadema Gerald John akitangaza kukihama chama hicho katika mkutano huo wa Mwembetogwa
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasluti wananchi waliokuwa
wakimshangilia alipowasili kwenye Viwanja vya Mwembetogwa, kuhutubia
mkutano huo wa hadhara Iringa mjini
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akiwasili kwenye
viwanja vya Mwembetogwa akitokea hospitali kupata matibabu baada ya
kuumia mkono wakati akicheza mpira leo asubuhi
Wananchi wakitoa ujumbe kupitia mabango kwenye mkutano huo wa Mwembetogwa mjini Iringa leo
Vijana
Chipukizi wa CCM, wakienda kwa ukakamavu kwenye mkutano huo wa hadhara
wa Kinana uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa leo.
Baadhi
ya viongozi na maofisa wa CCM wakishiriki na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kula chakula cha mchana kwa Mamalishe mjini Iringa
leo kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanjavya
Mwembetogwa leo
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akila chakula cha mchana kwa Mamalishe,
mjini Iringa leo, kabla ya kwenda kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye
Viwanja vya Mwembetogwa. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa, Jesca Msambatavangu
Mamalishe akimnawisha Kinana baada ya kula
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la madereva wa
daladala, wakereketwa wa CCM Iringa mjini kabla ya kwenda kuhutubia
mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Mwembetogwa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa SACCOS ya Masoko Vicoba, mjini Iringa leo
Kinana akiwasalimia wanachama wa Saccos hiyo alipoingia ukumbini kuzungumza nao mjini Iringa leo asubuhi
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kabla ya kuingia kwenye mkutano wa Wana-Saccos hao mjini Iringa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wakereketwa wa CCM eneo la Kihesa Mwang'ingo leo asubuhi
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wazee, alipotembelea shina
namba moja la Lucas Mkazizi eneo la Mkimbizi, Iringa Mjini leo asubuhi.
Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu
akisalimia kinamama
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpatia maji Mjumbe wa Shina namba
moja, Lucas Mkazizi, wakati yeye na msafara wake walipokunywa chai ya
asubuhi nyumbani kwa mjumbe huo baada ya kikao cha shina hilo
Kinana akinywa chai nyumbani kwa balozi huyo, mtaa wa Mkimbizi, Iringa mjini
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaslimia watoto wa kituo cha kulea
watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Upendo Centre, waliofika
kumlaki kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini leo asubuhi
Watoto wakiwa katika mapokezi hayo ya Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akilakiwa na wananchi alipowasili kwenye
Ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini leo asubuhi. Picha zote na Bashir
Nkoromo-CCM Blog Kwa Hisani ya Sufyan Omar
No comments:
Post a Comment