Mheshimiwa Sophia
Mfaume, MNEC Kupitia Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM TAIFA)
amewasihi watanzania Kuendelea na Muungano wa Serikali Mbili, alitoa
Utafiti mfupi alioufanya kuusiana na mchakato wa katiba mpya. alisema "Idadi ya watanzania wote kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 ni zaidi ya milioni 40.
Wananchi waliobahatika kutoa maoni katika tume ya kukusanya maoni kwa
ajili ya mchakato wa kuunda katiba mpya ni 778,211...kati yao
walioongelea muundo wa muungano ni wananchi elfu 47 sawa na 13% ya waliotoa maoni. Sasa kwa wale wanaojaribu kuudanganya umma kwamba watanzania wengi (13%) wanataka serikali 3 hayo mumeyatoa wapi??? Watanzania wanataka huduma bora, haki zao kuheshimiwa na kutekelezwa, kupungua kwa ukali wa maisha na maisha bora kwa ujumla. Tuache kuudanganya watanzania." | |
No comments:
Post a Comment