Pages

Ads 468x60px

Saturday, May 10, 2014

KINANA AWATEMBELEA WAFANYABIASHARA SOKONI IGUNGA

  • Kinana awatembelea wafanyabiashara soko kuu Igunga 
  • Azungumza nao na kujua changamoto zao
  • Asisitiza viongozi wengine kuwa karibu na wananchi na kuwasikiliza 
  • Kuanza ziara leo wilaya ya Nzega
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mfanyabiashara katika soko kuu la Igunga baada ya kumaliza mkutano wake kwenye kiwanja cha Sokoine jana jioni tarehe 9 Mei 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia tangawizi katika soko kuu la Igunga ,Katibu Mkuu alipita sokoni hapo kuwasalimia wauzaji na kuzungumza nao baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara kwenye kiwanja cha Sokoine Igunga mjini jana tarehe 9 Mei 2014.
 Mfanyabiashara wa Soko la Igunga akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Igunga ndugu Elibariki Kingu na kumuambia soko hilo linahitaji mitaro ya kupitisha maji ya mvua sokoni hapo mbele ,wengine pichani ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye jana tarehe 9 Mei 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichagua Nanasi kwenye soko la Kuu la Igunga mwingine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abrahman Kinana akikatiza katikati ya soko kuu la Igunga jana jioni baada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Sokoine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya matango kutoka kwa akina mama wafanyabiashara soko kuu la Igunga ,Katibu Mkuu alipita kuwasalimia na kuzungumza na wafanyabiashara sokoni hapo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment