SHUNYANGA, Tanzania
Diwani
wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga, Kasanga Lumala (75) amefariki dunia baada ya kuugua kwa
muda mrefu kifua kikuu.
Taarifa
iliyopatikana kutoka mjini Shinyanga, imesema, diiwani huyo
alifariki jana mida ya saa 10 jioni katika hospitali ya mkoa alikokuwa
amelazwa kwa muda wa siku mbili baada ya kuzidiwa akiwa
nyumbani wakati akiendelea kutumia dawa .
Kaimu
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ngassa Sosthenes amesema hayo,
akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga na kufafanua kwamba
katika uhai wake diwani huyo alisumbuliwa na maradhi ya ugonjwa huo wa
kifua kikuu licha ya kwamba alikuwa akipata katika
hospitali mbalimbali.
Alisema,
Desemba 26 mwaha huu, walipata taarifa ya kuzidiwa kwa diwani huyo
wakaamua kumpeleka haraka katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na
ndugu zake na madaktari kuendelea kumfanyia uchunguzi zaidi.
Amesema
leo mwili umetolewa hospitali na kuumpeleka kwenye kata yake kwa
ajili ya wananchi kwenda kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi kwenda
kufanyika mkoani Geita katika kata ya Mlele walikozikwa pia wazazi
wake.
Kwa
mujibu wa Kaim Kwenyekiti huyo wa Halmashauri, Diwani huyo aliyezaliwa
mwaka 1937, ameacha watoto saba wajane wawili na amekuwa diwani wa kata
hiyo kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2005.
Msiba
wa diwani huyo umekuja huku msiba mwingine wa Diwani wa kata ya
Nyida ukiwa bado unaombolezwa na wananchi kufuatia diwani
nao Mshindikwa Masele (40) kufariki dunia kutokana na ajali ya
pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha akitokea Isaka wilayani Kahama
Desemba 21, mwaka huu.





No comments:
Post a Comment