Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 18, 2014

VUAI AUPONGEZA UONGOZI WA TAWI LA CCM DMV MAREKANI KWA KUFANIKISHA UCHAGUZI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai (pichani)  aupongeza uongozi wa Tawi, CCM  DMV Marekani kwa kufanikisha uchaguzi wa Katibu wa Tawi.

Naibu katibu Mkuu Zanzibar alitoa pongezi hizo leo kupitia kwa Katibu Mwenezi, bi Salima Moshi, alisema anupongeza uongozi wa Tawi hilo, wajumbe wa Halmashauri kuu yaTawi, Msimamizi wa uchaguzi, ambaye alikuwa, kada Seif Akida alitokea Tawi la New York.

Aliwapongeza pia Wagombea wote kwa kujitokeza huku akimpongeza kwa dhati  mgombea aliyeshinda, na kuwatakia kila la kheri Wanachama wote wa CCM DMV Marekani.

Uongozi wa CCM DMV Marekani nao umesema unashukuru uchaguzi umekwisha salama na kusema "tuendeleze mshikamano wetu Umoja Wetu, ili kuweza kufanikisha shughuli zetu, KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment