Rais wa TFF Bw.
Jamal Malinzi akiwa na Dida Mushi Golikipa wa timu ya Taifa na Jorgen
Holdasen Mkurgenzi mkazi wa Plani International hapa nchini wakiwa
wameshika majarida mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari
kwenye ofisi za TFF jijini Datr es salaam
...................................................................................
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NDOA
za utotoni zinawazuia mamilioni ya watoto wa kike nchini wasiweze
kumaliza shule, kufikia ndoto zao katika maisha na kuwafanya waendelee
kuteseka katika umasikini.
Kuna
`mijibaba` inayoharibu watoto wa kike bila huruma na kama haitoshi
inaamua kufunga ndoa za `kihuni` na watoto ambao ni taifa la kesho.
Serikali
na mashiriki binafsi ya kutetea haki za watoto yanapambana dhidi ya
tatizo hili, huku wazazi na watu wazima wakiwa sehemu ya tatizo.
Mpira
wa miguu ni mchezo unaoongoza kuwa na mashabiki wengi nchini na dunia
kote, hivyo mchezo huu unaweza kutumika kama njia ya kupambana na ndoa
za utotoni.
Kwa
kutambua mchango unaoweza kuletwa na mpira wa miguu, shirikisho la soka
Tanzania, TFF limeingia ubia na shirika la kutetea haki za watoto la
`Plan International` kwa ajili ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi
wa haki za mtoto hapa nchini.
Mkataba
wa ushirikiano umesainiwa leo katika ofisi za TFF makao makuu jijini
Dar es salaam baina ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi na mkurugenzi wa `Plan
International Tanzania`, Jorgen Haldorsen . Ushirikiano huo una lengo
la kufanya kazi pamoja katika kushughulikia masuala ya ukatili wa
kijinsia, ndoa na mimba za utotoni.
Kwa
mujibu wa Bw. Haldorsen, soka ndio mchezo unaongoza nchini na duniani
kote kuwa na mashabiki wengi na kwamba joto la kombe la dunia
linaloendelea kule Brazil na namna watanzania wanavyofuatilia kupitia
luninga na wengine wakiwa Brazil ni ushahidi tosha.
“Tunatambua
uwezo wa mchezo huu kuwajumuisha watu. Sasa tunataka tuwajumuishe watu
sio tu kwa ajili ya furaha, pia kama njia ya kuleta mabadiliko juu ya
usawa wa kijinsia kwa kutetea na kuhamasisha juu ya haki za mtoto wa
kike”. Alisema Haldorsen.
Mkurugenzi
huyo wa `Plan International Tanzania` alidokeza kuwa ushirikiano na TFF
ni sehemu ya kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na shirika hilo
ulimwenguni inayoitwa `Because I Am A Girl`-BIAAG au kwa Kiswahili-KWA
SABABU MIMI NI MSICHANA ambapo inalenga kuwatoa mamilioni ya wasichana
kutoka katika umaskini kupitia uhamasishaji juu ya haki zao, elimu na
stadi za maisha.
“Kwa
kupita ubia huu tutakuwa na uwezo wa kuwafikia mamilioni ya Watanzania
na tutawapa wasichana ujumbe kuwa KWA SABABI MIMI NI MSICHANA, lazima
nipate fursa sawa na wavulana. KWA SABABU MIMI NI MSICHANA, lazima niwe
na uwezo wa kufunga magoli kufikia ndoto zangu katika maisha”. Alieleza
Bwa.Haldorsen.
Kwa
upande wake, Rais wa TFF ambaye ni mjumbe wa kamati ya Huduma kwa jamii
ya Shirikisho la mpira wa miguu Ulimwenguni, FIFA, alisema ubia huo ni
sehemu ya utekelezaji wa sera za huduma kwa jamii ya TFF na wana furaha
kushirikiana na Plan International kwa lengo hili muhimu.
“Ushirikiano
huu ni muhimu sana kwetu kwani unakileta chombo kikubwa kabisa cha
michezo hapa nchini pamoja na shirika la kutetea haki za watoto (plan
International) hususani kwa ajili ya haki za mtoto wa kike. Tunategemea
kutumia mtandao wetu nchi nzima kuelimisha juu ya usawa wa kijinsia na
uhamasishaji wa haki za mtoto wa kike,” . Alisema Rais Malinzi.
KUHUSU
PLAN INTERNATIONAL: Plan International ni shirika la kimaendeleo la
misaada ya kibinadamu, linalomlenga mtoto lisilofungamana na mrengo
wowote wa kidini, kisiasa au kiserikali.
Plan
International ilianzishwa zaidi ya miaka 70 iliyopita na inaendesha
shughuli zake katika nchi 70 duniani. Plan International imekuwa
inafanyakazi hapa Tanzania tangu mwaka 1991 ikiwasaidia watoto na jamii
kupata huduma za afya, elimu, maji, usafi na mazingira, kujikimu na
ulinzi. Inaendesha miradi Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Geita, Pwani,
Mwanza na Rukwa.
KAMPENI
YA KWA SABABU MIMI NI MSICHANA –BIAAG: Kampeni ya Kwa Sababu Mimi ni
Msichana-BIAAG (2012-2016) ni kampeni ya Plan ulimwenguni kote
inayolenga kuelimisha na kutetea haki za mtoto wa kike na kuwatoa
mamilioni ya wasichana kutoka kwenye lindi la umaskini kupitia elimu na
utoaji wa stadi za maisha na kazi.
Kampeni
hii inalenga kupambana na ubaguzi wa kijinsia na kuboresha maisha ya
wasichana milioni 4 duniani na zaidi ya laki 3 hapa Tanzania kwa
kuwawezesha kujiunga shuleni, kupata stadi za kiufundi na maisha,
kujikimu, na kushiriki katika shughuli mbalimbali katika jamii na
kulindwa, kwa kukabiliana na vikwazo dhidi ya maendeleo ya mtoto wa
kike.





No comments:
Post a Comment