Habari
zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka jijini Arusha, zinasema kuwa
abiria zaidi ya 200 waliokuwa ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege aina
ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines)
wamenusurika mchana wa leo baada ya ndege hiyo kushindwa kutua kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu
iliyojitokeza kwa dharula Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula
kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha.
Imeelezwa
kuwa kutokan na dharula hiyo ndege hiyo imelazimika kusimama nje ya
uwanja wa Arusha baada ya kushindwa kusimama kutokana na uwanja huo kuwa
mdogo.





No comments:
Post a Comment