Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akisindikizwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt.
Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe Bernard Membe kuelekea ukumbini kutunukiwa Shahada Ijumaa Septemba
20, 2013.
Nyimbo
za taifa zikipigwa wakati wa sherehe za kumtunuku Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aki Shahada ya
Uzamivu katika Chuo Kikuu Guelph jimboni Ontario, Canada, Ijumaa
Septemba 20, 2013.
Sehemu
ya umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu
ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo
Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso , Ijumaa Septemba
20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akishangiliwa katika Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada ya
Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20,
2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya
Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya
kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario
Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
Umati
ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu
cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na Wakuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa
Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa
Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akipongezwa baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha
Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru
Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu
cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Ijumaa, Septemba 20, 2013, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo
Kikuu cha Guelph katika jimbo la Ontario nchini Canada kwa kutambua
mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
Viongozi
wa Chuo hicho wanasema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete
kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili
kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio
makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania
na Afrika.
Rais
Kikwete ambaye amewasili Canada usiku wa Alhamisi, Septemba 19, 2013
akitokea Washington, D.C., Marekani ambako alikuwa kwa siku mbili
akitokea Jimbo la California amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa
shahada ya juu kabisa katika historia ya Chuo hicho.
Chuo
cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada
na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha
Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
Chuo
hicho ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na ubora wa shughuli zake
za utafiti kimekuwa katika mstari wa mbele kutafuta majawabu ya
changamoto zinazoikabili dunia katika masuala ya kilimo, raslimali za
maji, matatizo makubwa ya magonjwa ya mimea, matatizo ya ukuaji haraka
wa miji duniani na changamoto za biashara za kimataifa.
Katika
miaka ya karibuni kufuatia tishio kubwa kimataifa la ongezeko la bei za
vyakula duniani na hasa katika nchi masikini, mabadiliko ya tabianchi,
ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, changamoto
za upatikanaji wa maji safi na salama duniani, kazi ya Chuo hicho
imeongezeka sana.
Chuo
hicho kimeichagua Tanzania kama nchi ya kufanya nayo kazi katika Afrika
kukabiliana na changamoto hizo na kimemtambua Rais Kikwete kutokana na
mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo katika miaka yote ya uongozi
wake na mipango yake ya kuboresha kilimo katika Tanzania kama ASDP,
Kilimo Kwanza na SAGCOT ambayo yote inasifiwa sana kimataifa.
Chuo
hicho kina mahusiano ya karibu na Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine
cha Mzumbe – Morogoro na UDOM – Dodoma. Kati ya mwaka jana na mwaka
huu, Chuo hicho kimetiliana saini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) na
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM).
Mara
nne kati ya Januari, mwaka jana, 2012 na Juni, mwaka huu, 2013, uongozi
wa Chuo hicho ukiongozwa na Rais na Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Alastair
Summerlee na Makamu wa Rais wa Utafiti Dkt. Kevin Hall umetembelea
Tanzania na kukutana na viongozi wa Serikali pamoja na wale wa Vyuo
Vikuu vya Dar Es Salaam na Sokoine cha Mzumbe, Morogoro.
Mbali
na ujumbe ambao unaongozana na Rais Kikwete, sherehe za kutunukiwa kwa
Kiongozi Mkuu huyo wa Tanzania pia zimehudhuriwa na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Jumuia ya Watanzania
wanaoishi Canada pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
20 Septemba, 2013
















No comments:
Post a Comment