Rais Msaafu Mzee Mkapa atoa ya Moyoni kuhusu Rais Ajaye.
Mwisho wa Siku Wenye Busara Hujiuliza Ni Nani Anakubalika? - Benjamin William Mkapa
Salaam;
Kama kawaida yake Rais Jasiri na asiyemumunya maneno leo kazungumza
mengi sana wakati akihojiwa na Runinga ya Citizen kwa njia ya simu.Rais
Msataafu Benjamin Mkapa alikuwa akihojiwa juu ya kifo cha Rais wa Zambia
Hayati Michael Chilufya Satta aliyefariki leo huko jijini London.
Mkapa alisema namnukuu "Satta hakuitwa King Cobra kimakosa alistahili
kutokana na uwezo wake ama wa kimaamuzi au wa kimsimamo. I am very sure
that Zambians and we as African Nations will always remember Mr. Satta.
Satta was always there for his people and our Continent at large. He
said and stand for what he believed to be true and achievable;
hesitation was never a good term to Satta.
So the pain I (We)
faced when we lost Mzee Nyerere, Mzee Nkhurumah, Mzee Mandela, Mzee
Kenyatta is the same we are facing today when we talk about Mr. Satta
(Suffice it to say that we lost another hero in our Continent) May His
Soul Rest in Eternal Peace.........."
Baada ya salaam hizo mwandishi alimuuliza Mhe. Mkapa vipi siasa zetu Afrika kama Rais mstaafu anaziona je?
Mkapa; Kawaida na sina kubwa la kusema japo kuna mengi yanatokea
mengine ya hovyo mathalan waafrika wazee wetu walipigania sana ukombozi
wetu ila nadhani wengi bado wana matatizo na wanahitaji kukombolewa
kifikra manake kuna wenzetu wanatumika pasipo kujua na kusababishia Nchi
zao kuingia ktk matatizo kama vita na wengi wao wameanza kujuta.
Hivyo ni lazma ifikie mahali watu waweze kujitambua na kujua ni yepi malengo mema kwa Bara letu ni yepi tunashinizwa......
Mwandishi kaendele kumuuliza Mhe. Rais Mstaafu Nchi yako mapema mwakani
mnatazamia kufanya uchaguzi na mengi yamesikika hasa kwa wanaojitokeza
na wengine kupewa adhabu kama Mwenyekiti wa CCM Mstaafu una lipi la
kusema manake hata Mwl. Nyerere naye nyakati kama hizi hakusita kusema
neno....
Mkapa; (Kicheko) nachelea kupata jibu sahihi ila niseme
CCM ni Chama kikongwe na kina hazina kubwa ya kutosha. Na Katiba ya
Chama chetu inaelezea kuhusu dhumuni ya Chama chetu kubwa ikiwa ni
kuhakikisha tunakamata dola kuanzia Serikali za mitaa mpaka Serikali
kuu.Sasa swali ni kwamva dola inakamatwa je?
Chama kama chama
lazma muwe mtu anayeuzika na kukubalika ktk jamii kwa utendaji wake,
haiba yake, wasifu wake (ndani ya chama na serikali) lakini vile vile
ushawishi wake......Haya mambo ya umri na kadhalika sisi hatukutazama
wakati huo ila si dhambi Vijana wakijitokeza manake hata wakati wangu
Rais wa Sasa Mhe. Kikwete na kina Lowassa walijitokeza na leo unaona
Kikwete ndiye Rais.
Wakati wangu Viongozi wenzangu wengi walihisi
na kuamini kuwa sikuwa namuunga n mkono lakini mwandishi nataka
nikuhakikishie hata kama mimi Ben Mkapa siko na Kikwete mwisho wa siku
Wananchama ndio watakaosema wewe humtaki ila sisi tuachie huyo
huyo......
Na hayo yalijitokeza mwaka 2005 Watu walimtaka Mhe.
Kikwete sasa mimi kuwa Mwenyekiti wa Chama hakunipi Mandate ya
kushindana na walio wengi na mliona alishinda kwa asilimia kubwa kweli
kweli.Hivyo CCM ina taratibu zake na wanajua nani anafaa manake siasa
hizi tuhuma zingine za kipuuzi kweli kweli sasa mkiendekeza tuhuma
mwishowe mnakuta mnabaki bila chama na kwenye Siasa mkianza kutuhumiana
hakuna wa kusimama....
Hivyo binafsi naamini Chama kitapata mtu
safi na mwenye nguvu yai kukisaidia Chama na serikali na kuendeleza yale
aliyoyaacha Mhe. Kikwete hakuna Chama duniani ambacho kinaona kabisa
flani atatuvusha halafu kimwache hakuna manake huko ni kukiua
Chama.Hivyo hata sisi vyombo vyetu vya ndani vilikuwa vinatueleza kabisa
kwamba flani yuko vizuri sana ila labda kuna haka katatizo sasa hako
katatizo tunakafanyia kazi kwa maslahi ya chama ya kwa maslahi ya huyo
ajaye. Naamini ndivyo ilivyo hata mpaka sasa tafiti zimefanyika na
naamini wamesikia watu wakisema wanamtaka nani na wakati wangu mimi
Mgombea alikuwa amaeshatungiwa nyimbo na watu mbali mbali wenye mapenzi
naye. Hivyo labda hata sasa yaweza kuwa hivyo....Waswahili walisema
nyota njema huonekana asubuhi.
Nimalizie kama nilivyosema ukongwe wa CCM na viongozi wake naamini watapata mtu bora na mwenye nia njema na Taifa hili.....
Mwandishi Mhe. Mkapa katika waliotajwa naamini yupo mmona ama wawili
ambao umeona wanaweza ama viatu vyako ama vya Mwinyi au vya Mwalimu au
vya Mhe. Kikwete shirikiana nasi Mhe......
Mkapa (Kicheko) Hapa
kwetu kuna kamati ya maadili (Mwandishi Kicheko) Mkapa anaendele mimi na
wenzangu sasa Kikatiba ni wazee washauri hivyo Vikao vya Chama ndivyo
vitakavyotuongoza......... Baada ya hapo nasi tunaenda na huyo huyo
Mhe. Mkapa naomba nikuulize swali la mwisho tumepata kusikia kumetokea
muunganiko wa Vyama huko Tanzania kama hapa Kenya hilo unaliona je??
Mkapa; Sijajua sera zao na makubalinao yao yakoje na bado sijaelewa
kama muungano ww COARD na JUBILEE twaweza kuufananisha na huu.......
Otherwise I'd like to wish them all the best.....Mwandishi (Kicheko)
Nakushukuru sana Mhe. Mkapa kwa muda wako na tunakutakia afya njema..
Mkapa; Ahsante sana
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI